Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 19 | Sitting 10 | Home Affairs | Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi | 128 | 2025-04-23 |
Name
Emmanuel Adamson Mwakasaka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tabora Mjini
Primary Question
MHE. ATHUMAN A. MAIGE K.n.y. MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA aliuliza:-
Je, upi mpango wa Serikali wa kulipa madeni ya wazabuni hasa ya Polisi na Magereza?
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua madeni wanayodai wazabuni mbalimbali wanaotoa huduma, ambapo kwa Jeshi la Polisi kiasi cha fedha shilingi 651,730,893,477.29 kinadaiwa na katika mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali imelipa kiasi cha fedha shilingi 3,188,596,251.62. Aidha, deni la wazabuni katika Jeshi la Magereza ni jumla ya shilingi 33,527,055,286.00/= na kiasi cha fedha shilingi 15,072,994,270.00 kimefanyiwa uhakiki na Hazina na kinachosubiriwa ni malipo kutoka Wizara ya Fedha.
Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kulipa madeni hayo kwa kadri ya upatikanaji wa fedha toka kwenye bajeti ya Serikali inayotengwa kila mwaka wa fedha. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved