Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 19 | Sitting 13 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 153 | 2025-04-28 |
Name
Latifa Khamis Juwakali
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ALLY M. KASSINGE K.n.y. MHE. LATIFA KHAMIS JUAKALI aliuliza:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kuwapatia vijana elimu kuhusu mikopo ya asilimia 10?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Mamlaka za Serikali za Mitaa zimekuwa zikitoa mikopo kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu inayotokana na 10% ya mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kuzingatia Kifungu cha 37A cha Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, Sura 290 na Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo kwa Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu za mwaka, 2024.
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Kanuni ya 38 ya Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo kwa Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu za mwaka 2024, Mamlaka ya Serikali ya Mitaa zinapaswa kutoa mafunzo kwa vikundi vinavyoomba na kupata mkopo ikiwemo masuala ya uwekaji wa akiba, uundaji wa vikundi vyenye tija, uongozi, usimamizi wa fedha, uendeshaji wa miradi na utoaji wa taarifa na usimamizi wa marejesho ya mikopo.
Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia Kanuni hiyo katika mwaka wa fedha 2024/2025, Mamlaka za Serikali za Mitaa zimetoa mafunzo kwa vikundi 2,827 vya vijana ambavyo vilipewa mikopo ya 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved