Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 13 Energy and Minerals Wizara ya Nishat 157 2025-04-28

Name

Nicodemas Henry Maganga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbogwe

Primary Question

MHE. NICODEMAS H. MAGANGA aliuliza:-

Je, lini Serikali itakamilisha usambazaji wa umeme wa REA kwa vitongoji ambavyo bado havijapatiwa umeme wa REA Mbogwe?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Jimbo la Mbogwe lina jumla ya vitongoji 335 ambapo kati ya hivyo, vitongoji 140 vimepatiwa umeme, vitongoji 82 Wakandarasi wanaendelea na utekelezaji wa miradi na vitongoji 63 zabuni imetangazwa ili kupata Wakandarasi wa kutekeleza kupitia Mradi wa Kupeleka Umeme Vitongojini Awamu ya Pili B. Aidha, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini itaendelea kutenga fedha ili kugharamia utekelezaji wa mradi wa kupeleka umeme katika vitongoji 50 vilivyosalia. Ahsante. (Makofi)