Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 43 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 549 2025-06-10

Name

Maimuna Ahmad Pathan

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MAIMUNA A. PATHAN aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga uzio kwa shule zilizopo maeneo hatarishi kwa kuwa shule nyingi za Mkoa wa Lindi hazina uzio?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya elimu nchini ikiwa ni pamoja na kujenga uzio katika shule mbalimbali za msingi kwa kuzipa kipaumbele shule zenye watoto wenye mahitaji maalum.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2022/2023 – 2023/2024 Serikali imetoa shilingi bilioni 5.57 kwa ajili ya ujenzi wa uzio katika shule 185 za watoto wenye mahitaji maalum, ikiwemo Shule ya Msingi Namakonde iliyoko Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa. Aidha, shilingi milioni 105.57 zimetumika kujenga uzio katika Shule za Sekondari Lindi Wasichana na Nachingwea Wasichana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali Kuu na Mamlaka za Serikali za Mitaa zitaendelea kutenga fedha za ujenzi wa uzio kwa ajili ya usalama wa wanafunzi na mali za shule kadiri ya upatikanaji wa fedha. (Makofi)