Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 43 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 559 2025-06-10

Name

Yahya Ally Mhata

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyumbu

Primary Question

MHE. YAHYA A. MHATA aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Nanyumbu pamoja na nyumba za watumishi? (Makofi)

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu imetoa eneo Kitalu F, kiwanja namba moja kilichopo Mtaa wa Mangaka chenye ukubwa wa mita za mraba 68,682 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Nanyumbu pamoja na nyumba za makazi ya askari. Serikali inatarajia kujenga Kituo kipya cha Polisi cha Daraja B, kitakachogharimu kiasi cha fedha shilingi 802,926,788. Fedha kwa ajili ya ujenzi zitatengwa kwenye bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2026/2027. Baada ya ujenzi kukamilika, Serikali itatenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za makazi ya kuishi askari polisi, ahsante. (Makofi)