Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 43 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 189 2025-04-30

Name

Daimu Iddi Mpakate

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduru Kusini

Primary Question

MHE. DAIMU I. MPAKATE aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga maghala ya kuhifadhia mazao Vijijini?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka wa fedha 2025/2026 mpaka 2029/2030 Serikali ina mpango wa kujenga maghala na vihenge yenye uwezo wa kuhifadhi tani 3,000,000 za chakula. Katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali imekamilisha ujenzi wa ghala za kisasa 20 za ngazi ya kijiji zenye uwezo wa kuhifadhi tani 47,000 katika Mikoa ya Dodoma, Babati, Tabora, Kigoma, Ruvuma, Simiyu, Mtwara, Geita, Mwanza na Morogoro. ahsante sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kutambua umuhimu wa maghala na vihenge katika kuimarisha usalama wa chakula nchini, kwa sasa zoezi la kufanya tathmini ya utambuzi wa ghala za umma na binafsi linaendelea. Zoezi hilo litakapokamilika litawezesha kutoa mwongozo wa namna bora ya uwekezaji wa ghala katika maeneo mbalimbali nchini.