Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 11 Finance Wizara ya Fedha 184 2025-02-11

Name

Ameir Abdalla Ameir

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

House of Representatives

Primary Question

MHE. ABDUL YUSSUF MAALIM K.n.y. MHE. AMEIR ABDALLA AMEIR aliuliza:-

Je, ni miradi gani ya umwagiliaji inayofadhiliwa na mashirika ya kimataifa ambayo Zanzibar inanufaika nayo?

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imenufaika na ufadhili wa mashirika ya kimataifa katika miradi ya umwagiliaji inayolenga kuongeza uzalishaji wa kilimo na kuboresha maisha ya wakulima wa Zanzibar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miongoni mwa miradi inayotekelezwa ni Mradi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Umwagiliaji Zanzibar, ambao unatekelezwa kwa ufadhili wa Benki ya Exim ya Korea ambapo umefadhiliwa kupitia mkopo wa awali wa Dola za Kimarekani 50,000,000 na mkataba wa nyongeza wa Dola za Kimarekani 18,100,000. Utekelezaji wa mradi huu umefikia 98% na unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 8 Juni, 2025.