Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 11 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 187 2025-02-11

Name

Maryam Azan Mwinyi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Chake Chake

Primary Question

MHE. DKT. THEA M. NTARA K.n.y. MHE. MARYAM AZAN MWINYI aliuliza:-

Je, Serikali imefikia wapi katika mpango wa ujenzi wa Chuo Kikuu kishiriki cha Mwalimu Nyerere pamoja na hosteli Pemba?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, mnamo mwaka 2022, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilikipa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere eneo lenye ukubwa wa hekta 11.2 katika eneo la Mtumbi Pujini, Chakechake, Pemba kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Kampasi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mwaka 2023 Serikali ilianza ujenzi kwa kuanza na madarasa 10 yenye uwezo wa kutumiwa na wanafunzi 1,800 ambapo ujenzi wake ulishakamilika. Serikali inaendelea na ujenzi wa awamu ya pili unaohusisha ujenzi wa jengo la utawala ambao umefikia 95% na ujenzi wa jengo la kumbi za mihadhara lenye uwezo wa kutumiwa na wanafunzi 1,000 kwa mara moja ambao umefikia 60%. Serikali inatarajia kukamilisha ujenzi huu mnamo Aprili, 2025.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kufuatia kukamilika kwa baadhi ya majengo, chuo kimeshaanza shughuli za utoaji wa mafunzo na ujifunzaji. Aidha, katika awamu zijazo Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa hosteli na miundombinu mingine katika chuo hiki. Ninakushukuru sana. (Makofi)