Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 19 | Sitting 39 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 498 | 2025-06-04 |
Name
Shabani Omari Shekilindi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lushoto
Primary Question
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI aliuliza: -
Je, lini Serikali itazipatia fedha za ukarabati Shule Kongwe za Msingi Makanya na Kwai katika Jimbo la Lushoto?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, Shule ya Msingi Makanya imechakaa kiasi cha kutokarabatika. Hivyo, katika mwaka wa fedha 2024/25 Serikali imetenga shilingi milioni 424.7 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mipya ambapo hadi Mei, 2025 shilingi milioni 96 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na matundu ya vyoo kumi.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2024/2025 Shule ya Msingi Kwai imetengewa shilingi milioni 202.2 kupitia Mradi wa BOOST kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu chakavu na ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na matundu ya vyoo kumi na mawili.
Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kutenga fedha za kukarabati au kujenga miundombinu mipya katika shule kongwe na chakavu kote nchini.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved