Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 39 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 502 2025-06-04

Name

Cecil David Mwambe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ndanda

Primary Question

MHE. ESTHER N. MATIKO K.n.y. MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza: -

Je, kwa nini Serikali isiagize CAG akague URA SACCOS ya Jeshi la Polisi?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, URA SACCOSS ni chama cha ushirika kilichosajiliwa na kinasimamiwa na kukaguliwa kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 6 ya mwaka 2013 na Sheria Namba 10 ya mwaka 2018 ya Huduma Ndogo ya Fedha na ni mali ya wanachama ambao ni watumishi wa Jeshi la Polisi. URA SACCOSS hukaguliwa kila mwaka na Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO), pia hukaguliwa na mrajisi wa vyama vya ushirika kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC). URA SACCOSS ni ushirika uliopata hati safi kuanzia mwaka 2015 hadi 2024, pia umepata tuzo ya SACCOSS bora nchini kuanzia mwaka 2021 hadi 2024, hii ni kutokana na kufuata sheria, kanuni na taratibu za ushirika na fedha na taarifa zake husomwa kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa wanachama kama matakwa ya sheria yanavyoelekeza, ahsante.