Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 39 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 511 2025-06-04

Name

Tumaini Bryceson Magessa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Primary Question

MHE. TUMAINI B. MAGESSA aliuliza: -

Je, Serikali ipo hatua gani kwenye ujenzi wa kipande cha barabara kutoka Katoro hadi Daraja la Nyikonga kwenye Barabara ya Katoro – Ushirombo?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imeanza taratibu za kuijenga barabara hii kwa kuanza na ujenzi wa Daraja ya Nyikonga ambapo zabuni kwa ajili ya kumpata mkandarasi wa ujenzi wa daraja ziko hatua za mwisho. Kwa upande wa barabara, upembuzi yakinifu na usanifu wa kina umekamilika na kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi.