Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 18 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 227 2025-05-06

Name

Eng. Ezra John Chiwelesa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Biharamulo Magharibi

Primary Question

MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga vituo vya kuegesha malori katika maeneo ya Nyakahura na Biharamulo Mjini?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2023/2024, Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo ilitoa shilingi milioni 20 kwa ajili ya kuanza matengenezo ya awali ya usawazishaji wa eneo na ujazaji wa kifusi katika maegesho ya malori Nyakahura. Aidha, katika mwaka wa fedha 2024/2025 halmashauri imetenga shilingi milioni 15 kwa ajili ya ujenzi wa choo. Maegesho haya yataanza kutumika kabla ya mwezi Julai, 2025.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa ujenzi wa maegesho ya malori Biharamulo Mjini. Katika mwaka wa fedha 2024/2025, halmashauri imetenga shilingi milioni tano kwa ajili ya kupima na kuandaa nyaraka za umiliki wa eneo lililopatikana katika Kata ya Nyamahanga kwa ajili ya ujenzi wa maegesho hayo.