Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 18 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 231 2025-05-06

Name

Abubakar Damian Asenga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilombero

Primary Question

MHE. ABUBAKARI D. ASENGA aliuliza: -

Je, lini Serikali itapunguza Mlima Mang’ula Kona Kilombero ikiwa ni ahadi ya Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, eneo la Mlima Mang’ula Kona ambalo liko Kilombero, kandokando mwa barabara ya Mikumi – Kidatu – Ifakara. Eneo hilo limeshafanyiwa ukaguzi na kazi ya usanifu ipo kwenye hatua za mwisho kwa ajili ya kupunguza ama kukata kipande cha mlima na uimarishaji wa kingo ili kuzuia maporomoko ya udongo wakati na baada ya kukata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi ya kupunguza mlima itaanza mara tu baada ya kukamilika usanifu na kumpata mkandarasi wa kutekeleza kazi hiyo, ahsante.