Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 22 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 278 2025-05-12

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Primary Question

MHE. JOSEPH M. MKUNDI K.n.y. MHE. JOSEPH G. KAKUNDA aliuliza:-

Je, lini Serikali itafikisha huduma za maji safi na salama katika shule zote za msingi na sekondari nchini?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Sensa ya Elimu Msingi Mwaka 2024 inaonesha kuwa shule 5,311 za sekondari zina vyanzo vya maji vya uhakika ambapo shule zenye maji ya bomba ni 2,960, shule zenye maji ya visima ni 1,217 na wanaovuna maji ya mvua ni shule 1,134. Aidha, shule 20,509 za msingi zina vyanzo vya maji ya uhakika ambapo shule zenye maji ya bomba ni 10,965, maji ya visima ni shule 4,966 na shule zinazovuna maji ya mvua ni 4,578.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mikakati ya Serikali ya kufikisha huduma za maji safi na salama katika shule za msingi na sekondari nchini ni pamoja na:-

Kuhakikisha kuwa ujenzi wa shule mpya unajumuisha fedha za ujenzi wa miundombinu ya maji inayohusisha kuvuna maji ya mvua; kuunganishwa na mifumo ya mamlaka za maji na kuchimba visima; Ujenzi wa miundombinu ya vyoo unajumuisha fedha ya ujenzi wa miundombinu ya maji tiririka; na kutumia sehemu ya fedha ya ruzuku ya uendeshaji wa shule kufanya ukarabati wa miundombinu ya maji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mamlaka za Serikali za Mitaa zitaendelea kuweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha shule zinakuwa na huduma ya maji safi na salama.