Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 3 Sitting 1 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 7 2016-04-19

Name

Ussi Salum Pondeza

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chumbuni

Primary Question

MHE. USSI SALUM PONDEZA AMJAD aliuliza:-
Kituo cha Polisi Maruhubi kinakabiliwa na matatizo mbalimbali kama vile ukosefu wa askari wa kutosha; kituo hakitoi huduma saa 24, lakini pia majengo yake ni machakavu sana kiasi kwamba hayana hadhi ya kuwa Kituo cha Polisi:-
(a) Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka askari wa kutosha katika kituo hicho na kuhakikisha kuwa kituo kinatoa huduma zake kwa saa 24?
(b) Je, ni lini Serikali itayakarabati majengo ya kituo hicho ili yaendane na hadhi ya Kituo cha Polisi?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, naomba nijibu swali la Mheshimiwa Ussi Salum Pondeza, Mbunge wa Chumbuni, kama ifuatavyo:-
(a) Mheshimiwa Spika, Kituo cha Polisi cha Maruhubi ni Kituo cha Daraja ā€œCā€ ambacho taratibu za utoaji huduma kwa mujibu wa miongozo ya Jeshi la Polisi kitatoa huduma kuanzia saa 12.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni na kuwa na askari wasiozidi 20.
(b) Mheshimiwa Spika, Serikali itakifanyia ukarabati Kituo cha Maruhubi mara tu fedha zitakapopatikana.