Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 11 Sitting 35 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 298 2018-05-23

Name

Nassor Suleiman Omar

Sex

Male

Party

CUF

Constituent

Ziwani

Primary Question

MHE. NASSOR SULEIMAN OMARY aliuliza:-
Uhakiki wa vyeti feki umeathiri wafanyakazi wengi na wengine wamepoteza ajira zao:-
Je, ni wafanyakazi wangapi wamepoteza ajira zao sekta ya elimu pekee?

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA) alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Nassor Suleiman Omar, Mbunge wa Ziwani, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2016/2017 na 2017/2018, Serikali ilifanya uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma ili kubaini waliokuwa na vyeti halali na waliokuwa na vyeti vya kughushi. Katika uhakiki huo, jumla ya Walimu 3,655 walibainika kuwa na vyeti vya kughushi, hivyo walipoteza sifa za kuendelea kuwa watumishi wa umma.