Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 11 Sitting 22 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 178 2018-05-04

Name

Kiswaga Boniventura Destery

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Magu

Primary Question

MHE. BONIVENTURA D. KISWAGA aliuliza:-
Serikali inaanzia katika ngazi ya kitongoji, mtaa na kijiji:-
Je, ni lini viongozi na Wenyeviti wa Vitongoji, Mtaa na Kijiji watalipwa mishahara?

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Boniventura Destery Kiswaga, Mbunge wa Magu, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, miongoni mwa sifa zinazomwezesha Mtanzania kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kijiji, Kitongoji au Mtaa ni pamoja na kuwa na shughuli halali inayomwingizia kipato. Kwa muktadha huo, utaratibu wa viongozi kwa ngazi hiyo kulipwa mishahara kama ilivyoulizwa katika swali la msingi haujawahi kuwekwa kwenye sheria yoyote.