Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2015-2020 | Session 15 | Sitting 25 | Information, Culture, Arts and Sports | Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo | 204 | 2019-05-10 |
Name
Livingstone Joseph Lusinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mtera
Primary Question
MHE. FELISTER A. BURA (K.n.y. MHE. LIVINGSTON J. LUSINDE) aliuliza:-
Kwa kuwa Serikali imehamia Dodoma, je, kwa nini Serikali isijenge Maktaba yenye kumbukumbu za kazi za Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo pia itakuwa sehemu ya utalii kwa watu wa ndani na nje ya Mkoa wa Dodoma?
Name
Juliana Daniel Shonza
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, napenda kjibu swali na Mheshimiwa Livingstone Lusinde, Mbunge wa Mtera, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kwa kuzingatia umuhimu wa kuhifadhi kumbukumbu za Waasisi wa Taifa ambao ni Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Hayati Abeid Aman Karume, ilitunga Sheria ya Kuwaenzi Waasisi ya mwaka 2004. Sheria hii inaelekeza uhifadhi wa kumbukumbu hizo na kuanzishwa kwa kituo cha kutunza kumbukumbu. Aidha, Umoja wa Afrika uliiteua Tanzania mwaka 2011 kuwa Mratibu wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika ambayo, pamoja na mambo mengine, imetoa kipaumbele katika uhifadhi wa kazi ambazo alifanya Baba wa Taifa na mashujaa wenzake katika ukombozi wa Afrika.
Mheshimiwa Naibu Spika, ni katika msingi huo Serikali kwa kushirikiana na UNESCO, imekarabati studio za iliyokuwa Redio Tanzania Dar es Salaam zilizopo barabara ya Nyerere na kuwa kituo adhimu cha kuhifadhi na rejea ya kazi za Baba wa Taifa. Serikali vilevile, inaunga mkono juhudi za taasisi kadhaa nchini katika kuhifadhi amali za urithi wa kumbukumbu za Baba wa Taifa. Baadhi ya taasisi hizo ni kama ifutavyo:-
Maktaba ya Taifa, Dar es Salaam; Makumbusho ya Taifa, Dar es Salaam; Makumbusho ya Mwalimu Nyerere, Butiama; Ofisi ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa; Taasisi ya Mwalimu Nyerere; na Vituo vya Television vya TBC na ITV.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika utekelezaji wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika, Serikali imeteua Wilaya ya Kongwa, Dodoma kuwa Kituo Kikuu cha Kumbukumbu za Ukombozi wa Nchi yetu ambapo miundombinu kadhaa ya uhifadhi wa historia itajengwa zikiwemo kazi adhimu za Baba wa Taifa. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved