Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2015-2020 | Session 18 | Sitting 2 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 15 | 2020-01-29 |
Name
Richard Mganga Ndassa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Sumve
Primary Question
MHE. RICHARD M. NDASSA (K.n.y. MHE. KISWAGA B. DESTERY) aliuliza:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kutumia mtandao wa maji Magu kupeleka Tarafa ya Ndagalu, Kata za Shishani, Njinjinili, Kabila, Nkungulu, Ng’haya, Sukuma, Buhumbi na Mwamabanza zenye jumla ya vijiji 24?
Name
Jumaa Hamidu Aweso
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Pangani
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kiswaga, Mbunge wa Jimbo la Magu, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa Maji Magu Mjini ambao tayari umekamilika, una uwezo wa kuzalisha maji kiasi cha lita milioni 7.25 kwa siku, ukilinganisha na mahitaji ya sasa ya lita milioni 3.54 kwa wakazi wa Magu Mjini na Vijiji vya Kipeja, Sagani, Nyashimba na Ilungu. Hivyo Mradi huu una ziada ya maji ya lita milioni 3.71 kwa siku kwa sasa kutokana na ziada hiyo, Serikali kupitia Programu ya lipa kwa matokeo yaani Programme for Results (P4R) itajenga miundombinu ya usambazaji wa maji kutoka kwenye Mradi wa Magu mjini kupeleka kwa baadhi ya vijiji vilivyopo tarafa ya Ndagalu ikiwa ni pamoja na Vijiji vya Misungwi, Kitongo, Lumeji, Buhimbi, Iseni, Nyang’hanga na Nyashoshi.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuhakikisha kuwa azma ya upatikanaji wa maji katika vijiji vingine vya Tarafa ya Ndagalu inapatiwa ufumbuzi wa kudumu, Serikali itahakikisha kuwa imetenga fedha katika bajeti ya Mwaka 2020/2021 ili vijiji vilivyobaki viweze kupata huduma ya maji kupitia Mradi wa Ziwa Victoria.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved