Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2015-2020 | Session 17 | Sitting 4 | Home Affairs | Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi | 50 | 2019-11-08 |
Name
Selemani Jumanne Zedi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bukene
Primary Question
MHE. SELEMANI J. ZEDI aliuliza:-
Kijiji cha Sojo katika Kata ya Isugule, Wilayani Nzega patajengwa Kituo kikubwa (coating yard) cha kuandaa mabomba yote ya mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima, Uganda hadi Chongoleani, Tanga ambapo Kituo hicho kitakuwa na wafanyakazi zaidi ya 2,000; kutokana na ongezeko hilo la idadi ya watu mahitaji ya huduma za Jamii yatakuwa makubwa:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kuanzisha Kituo kidogo cha Polisi katika Kijiji cha Sojo ili kuhakikisha usalama kwa wananchi na mali zao?
Name
Eng. Hamad Yussuf Masauni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kikwajuni
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Selemani Jumanne Zedi, Mbunge wa Bukene, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Jeshi la Polisi iliona umuhimu wa kuwepo kwa Kituo cha Polisi katika Kijiji cha Sonjo ambapo ndipo kitakapojengwa kituo cha kuandaa mabomba ya mafuta toka Uganda kuja Tanzania. Aidha, juhudi mbalimbali zimekwishaanza ambapo Uongozi wa Polisi Mkoa wa Tabora kwa kushirikiana na Uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega wanaendelea na utaratibu wa kupata eneo la kujenga Kituo cha Polisi kitakachokuwa na hadhi ya daraja āCā ambacho kitakuwa na Askari kuanzia kumi na tano (15), pia eneo la ujenzi wa nyumba za kuishi askari.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa wananchi wa Sonjo wanapata huduma ya Polisi katika Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Nzega.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved