Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 4 | Sitting 5 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 61 | 2021-09-06 |
Name
Maryam Azan Mwinyi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Chake Chake
Primary Question
MHE. MARYAM AZAN MWINYI Aliuliza: -
Je, Serikali haioni haja ya kuwa na Mtaala mmoja kuanzia Kidato cha Kwanza hadi cha Nne kati ya Tanzania Bara na Zanzibar? (Makofi)
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA Alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Maryam Azan Mwinyi Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikishirikiana vizuri na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika masuala mbalimbali ikiwemo suala la elimu hususan katika utekelezaji wa mitaala na kutoa elimu bora kwa watoto wa kitanzania.
Mheshimiwa Spika, katika utekelezaji wa mitaala ya elimu kati ya Tanzania Bara na Visiwani, pande zote mbili hutumia mtaala mmoja kuanzia Kidato cha Kwanza hadi Kidato cha Sita. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved