Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 3 | Sitting 52 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 434 | 2021-06-16 |
Name
Nicholaus George Ngassa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Igunga
Primary Question
MHE. NICHOLAUS G. NGASSA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Chuo cha VETA Igunga?
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia naomba kujibu swali la Mheshimiwa Nicholaus George Ngassa, Igunga kama ifuatavyo: -
Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Igunga ni miongoni mwa vyuo 29 ambavyo vinaendelea kujengwa. Ujenzi wa Chuo hiki unaendelea vizuri na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Julai, 2021. Aidha, mchakato wa ununuzi wa mitambo na zana za kufundishia unaendelea sambamba na ukamilishwaji wa chuo hiki. Ujenzi wa chuo hiki utakapokamilika udahili wa wanafunzi wa kozi fupi utaanza mara moja wakati ule wa kozi ndefu unatarajia kutafanyika ifikapo Januari, 2022. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved