Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 6 | Sitting 10 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 115 | 2022-02-14 |
Name
Minza Simon Mjika
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MINZA S. MJIKA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itajenga Chuo cha VETA katika Wilaya ya Meatu?
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia napenda sasa kujibu swali la Mheshimiwa Minza Simon Njika, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea kujenga Vyuo vya VETA katika Mikoa na Wilaya mbalimbali kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha kwa lengo la kuongeza fursa za upatikanaji wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi nchini. Kwa sasa Serikali inaendelea na ujenzi wa vyuo vya VETA katika Wilaya 25 na Mikoa 4 ukiwemo Mkoa wa Simiyu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi ambacho Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha VETA katika Wilaya ya Meatu na maeneo mengine, wananchi wa Meatu wanashauriwa kutumia Vyuo vya VETA na Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi vilivyopo jirani kwa ajili ya kupata elimu na mafunzo ya ufundi. Nakushukuru.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved