Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 6 | Sitting 10 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Waziri wa Mifugo na Uvuvi | 118 | 2022-02-14 |
Name
Deus Clement Sangu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kwela
Primary Question
MHE. DEUS C. SANGU aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga mialo katika Forodha za Nankanga na Ilanga zilizopo ndani ya Ziwa Rukwa ili kurahisisha shughuli za Uvuvi?
Name
Abdallah Hamis Ulega
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkuranga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Deus Clement Sangu, Mbunge wa Kwela, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, mpango mkakati wa Serikali ni kuhakikisha inajenga na kuboresha mialo katika maeneo mbalimbali nchini yanayojishughulisha na shughuli za uvuvi ikiwemo maeneo yanayozunguka Ziwa Rukwa kama vile forodha za Nankanga na Forodha ya Ilanga. Aidha, utekelezaji wa mkakati huu unategemea upatikanaji wa rasilimali fedha.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved