Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 6 Sitting 12 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Waziri wa Mifugo na Uvuvi 142 2022-02-16

Name

Kenneth Ernest Nollo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bahi

Primary Question

MHE. KENNETH E. NOLLO aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga kituo cha uzalishaji wa madume bora ya ng’ombe Wilayani Bahi ili kuleta tija kwa wafugaji?

Name

Abdallah Hamis Ulega

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkuranga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kenneth Ernest Nollo, Mbunge wa Bahi, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, mpango wa Serikali ni kuimarisha mashamba yake ya uzalishaji wa madume bora ya Mabuki, Mwanza; Kitulo, Njombe; na Sao Hill lililopo Mkoani Iringa ili yaweze kuzalisha madume mengi na bora kwa lengo la kuyasambaza kwa wafugaji wote wanaohitaji ikiwa ni pamoja na wafugaji wa Wilaya ya Bahi.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia Serikali inaendelea kusisitiza matumizi ya teknolojia ya uhimilishaji katika kuboresha kosaafu za ng’ombe ili kuwa na kundi la mifugo yenye tija katika kuzalishaji nyama na maziwa na hivyo kukidhi mahitaji ya soko.