Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 8 | Sitting 1 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 17 | 2022-09-13 |
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Primary Question
MHE. DUNSTAN L. KITANDULA aliuliza: -
Je, ni lini ujenzi wa Chuo cha VETA unaoendelea Wilayani Mkinga utakamilika?
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -
Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Sayansi na Teknolojia, naomba sasa kujibu swali la Mheshimiwa Dunstan Luka Kitandula, Mbunge wa Mkinga, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wa kukamilika kwa Chuo cha VETA cha Wilaya ya Mkinga pamoja na vyuo vingine ili viweze kutoa mafunzo yatakayowawezesha vijana wetu kujiajiri na kuajiriwa. Kwa sasa ujenzi wa Chuo hiki upo katika hatua za mwisho za ukamilishaji ambapo ujenzi umefikia asilimia 95. Ujenzi wa Chuo hiki unatarajiwa kukamilika kabla ya mwezi Disemba, 2022. Hivyo, Chuo hiki kinatarajiwa kuanza kutoa mafunzo ya muda mfupi kuanzia mwezi Oktoba, 2022 na mafunzo ya muda mrefu mwezi Januari, 2023. Nakushukuru. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved