Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 8 | Sitting 8 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 131 | 2022-09-22 |
Name
Husna Juma Sekiboko
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HUSNA J. SEKIBOKO aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaifanya elimu ya sekondari kuwa ya lazima?
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -
Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Husna Juma Sekiboko, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali inafanya mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 kwa lengo la kuiboresha elimu yetu ili iweze kukidhi mahitaji ya sasa na baadaye.
Mheshimiwa Spika, kwa sasa Serikali ipo katika hatua ya kupokea na kuchambua maoni ya wadau kuhusu Sera ya Elimu, hivyo suala la elimu ya sekondari kuwa ya lazima itategemea maoni ya wadau na mahitaji ya wakati. Rasimu ya kwanza ya Sera ya Elimu inatarajiwa kukamilika mwezi Disemba, 2022. Nakushukuru.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved