Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 8 | Sitting 8 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 132 | 2022-09-22 |
Name
Esther Nicholus Matiko
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTHER N. MATIKO aliuliza: -
Je, kwa takwimu ni wahitimu wangapi wa kada ya Ualimu wa masomo ya sayansi na hesabu hawajaajiriwa tangu mwaka 2015?
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -
Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, naomba kujibu Swali la Mheshimiwa Esther Nicholaus Matiko, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, tangu mwaka 2015 hadi 2022 jumla ya wahitimu 33,492 wa kada ya Ualimu wa Masomo ya Sayansi na Hisabati wamehitimu mafunzo katika Vyuo mbalimbali vya Ualimu na Vyuo Vikuu. Kati yao wahitimu 13,383 wameajiriwa katika shule mbalimbali nchini tangu mwaka 2015. Aidha, wahitimu 20,109 hawajaajiriwa katika shule za Serikali.
Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kuajiri ili kukidhi mahitaji ya Walimu katika shule za umma. Nakushukuru sana.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved