Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 8 | Sitting 4 | Lands, Housing and Human Settlement Development | Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi | 52 | 2022-09-16 |
Name
Zuberi Mohamedi Kuchauka
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Liwale
Primary Question
MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA aliuliza: -
Je, Serikali ipo tayari kufanya mapitio ya upimaji wa vijiji nchini kwa kuwa migogoro mingi imesababishwa na upimaji usio shirikishi wa mwaka 1970?
Name
Ridhiwani Jakaya Kikwete
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chalinze
Answer
NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Zuberi Mohamed Kuchauka, Mbunge wa Liwale, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kumfahamisha Mheshimiwa Mbunge kabla ya kujibu swali lake la msingi kuwa kilichofanyika katika miaka ya 1970 haikuwa upimaji wa vijiji bali ilikuwa ni Operesheni Maalum ya Serikali ya kuanzisha Vijiji vya Ujamaa nchini.
Mheshimiwa Naibu Spika, miaka ya 2000 Serikali ilitekeleza Programu ya upimaji wa vijiji kwa lengo la kuvifanya vijiji kuwa mamlaka kamili za usimamzi wa ardhi za vijiji. Mathalani, katika Mkoa wa Lindi jumla ya vijijii 401 kati ya vijiji 523 vikiwemo Vijiji vya Wilaya ya Liwale vilipimwa kwa njia shirikishi na kuwekewa alama za mipaka.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved