Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 8 | Sitting 4 | Community Development, Gender and Children | Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum | 63 | 2022-09-16 |
Name
Jesca Jonathani Msambatavangu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Iringa Mjini
Primary Question
MHE. DKT. RITTA E. KABATI K.n.y. MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU aliuliza: -
Je, Serikali ipo tayari kuanzisha shule maalum kikanda ili kusaidia watoto walioathirika na ukatili wa kijinsia?
Name
Dr. Dorothy Onesphoro Gwajima
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Nominated
Answer
WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Jesca Jonathan Msambatavangu, Mbunge wa Iringa Mjini kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua umuhimu wa kuwasaidia Watoto manusura wa ukatili, ambapo imeweka mifumo mbalimbali ikiwemo; Kamati za Jamii za Ulinzi wa Wanawake na Watoto; Madawati ya Jinsia kwenye Vituo vya Jeshi la Polisi na Magereza; Vituo vya Mkono kwa Mkono kwenye Hospitali; Madawati ya Jinsia Vyuo Vikuu na Kati; Madawati ya Ulinzi wa Watoto Shule za Msingi na Sekondari; pia Nyumba Salama kwa ajili ya Manusura kupata huduma jumuishi.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved