Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 9 | Sitting 3 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 42 | 2022-11-03 |
Name
Geoffrey Idelphonce Mwambe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Masasi Mjini
Primary Question
MHE. GEOFFREY I. MWAMBE aliuliza: -
Je ni lini serikali itajenga Chuo cha Ualimu Masasi baada ya Chuo cha Ualimu Ndwika kuwa shule ya Sekondari ya Wasichana?
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -
Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Geoffrey Idelphonce Mwambe, Mbunge Jimbo la Masasi, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali ilibadili Chuo cha Ualimu Ndwika kuwa Shule ya Sekondari ya Wasichana kutokana na mahitaji ya wakati huo. Kwa sasa Serikali ina vyuo 35 vya Ualimu vyenye uwezo wa kudahili wanachuo 25,054 ambapo hadi sasa jumla ya wanachuo 22,085 wamesajiliwa. Idadi hii ni chini ya uwezo wa vyuo hivyo katika udahili kwa ujumla.
Mheshimiwa Spika, kwa sasa Serikali imeelekeza nguvu katika ukarabati wa vyuo hivyo ili kuweka mazingira wezeshi ya ufundishaji na ujifunzaji. Aidha, Serikali itaendelea kujenga Vyuo vya Ualimu katika maeneo mbalimbali kulingana na mahitaji na rasilimali.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved