Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 9 | Sitting 4 | Justice and Constitutional Affairs | Wizara ya Katiba na Sheria | 61 | 2022-11-04 |
Name
Vincent Paul Mbogo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nkasi Kusini
Primary Question
MHE. VINCENT P. MBOGO aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itafanya ukarabati wa Mahakama ya Mwanzo Chala?
Name
Geophrey Mizengo Pinda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kavuu
Answer
NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Vincent Paul Mbogo, Mbunge wa Nkasi Kusini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Tarafa ya Chala yenye Kata nne; za Chala, Nkadasi, Kipande na Mkwamba, ina Mahakama za mwanzo mbili za Chala na Kipande. Katika kuimarisha majengo ya Mahakama kwa kuzingatia mpango uliopo wa ujenzi na ukarabati wa Mahakama nchini, Mahakama ina mpango wa kukarabati jengo la Mahakama ya Mwanzo Chala katika mwaka wa fedha 2024/2025.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved