Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 9 | Sitting 6 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Waziri wa Mifugo na Uvuvi | 78 | 2022-11-07 |
Name
Stella Simon Fiyao
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza: -
Je, kuna mkakati gani wa kuzuia nyavu haramu?
Name
Abdallah Hamis Ulega
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkuranga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Stella Simon Fiyao, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Wizara imeandaa Mkakati wa Kusimamia Rasilimali za Uvuvi ambao unajumuisha mbinu mbalimbali za kudhibiti utengenezaji, uagizaji, matumizi na biashara ya nyavu haramu za uvuvi. Utekelezaji wa mkakati huo unahusisha wadau mbalimbali ikiwemo vyombo vya ulinzi na usalama, sheria, watendaji wa taasisi zilizopo mipakani, bandarini na viwanja vya ndege; Viongozi wa Mikoa na Wilaya, wavuvi pamoja na watendaji wa Wizara kupitia vituo vya ulinzi wa rasilimali za uvuvi. Aidha, elimu kwa wadau kuhusu matumizi ya nyavu sahihi, uvuvi endelevu na wenye tija inaendelea kutolewa. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved