Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 9 | Sitting 10 | Works, Transport and Communication | Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi | 146 | 2022-11-11 |
Name
Elibariki Emmanuel Kingu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Singida Magharibi
Primary Question
MHE. SHALLY J. RAYMOND K.n.y. MHE. ELIBARIKI I. KINGU aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya kutoka Singida hadi Sepuka kuelekea Kizaga itajengwa kwa kiwango cha lami katika Wilaya ya Ikungi?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Elibariki Immanuel Kingu, Mbunge wa Singida Magharibi, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali imekamilisha usanifu wa kina na maandalizi ya nyaraka za zabuni kwa barabara ya Sabasaba – Sepuka – Ndago hadi Kizaga yenye urefu wa kilometa 77.6 na inategemea kutangaza zabuni kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami mwishoni mwa mwezi Novemba, 2022. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved