Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 7 | Sitting 4 | Works, Transport and Communication | Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi | 38 | 2022-04-11 |
Name
Naghenjwa Livingstone Kaboyoka
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza: -
Je, ni nani mwenye jukumu la kusafisha mifereji na kuzibua makaravati ya barabara zinazojengwa chini ya TARURA au TANROADS?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Naghejwa Livingstone Kaboyoka, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, jukumu la usafi wa barabara na mifereji ikiwa ni pamoja na kuzibua makaravati ni la msimamizi wa barabara husika. Hivyo, kwa barabara za TANROADS mhusika ni TANROADS na za TARURA mhusika ni TARURA.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved