Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 9 | Sitting 7 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 96 | 2022-11-08 |
Name
Dr. Paulina Daniel Nahato
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. PAULINA D. NAHATO aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itawalipa Wahadhiri wote nchini malimbikizo yao ya miaka ya nyuma?
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Paulina Daniel Nahato, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali hulipa malimbikizo ya watumishi wote wa Serikali wakiwemo Wahadhiri baada ya kujaza fomu za malimbikizo (arrears clearance forms). Mara baada ya mtumishi kukamilisha kujaza fomu hizo na kuwasilishwa, madai yao hupelekwa Ofisi ya Rais, Management ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na baadaye Hazina kwa ajili ya malipo.
Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Septemba, 2022, Serikali imelipa jumla ya Sh.1,172,429,710 kwa ajili ya malimbikizo ya Wahadhiri. Serikali itaendelea kulipa malimbikizo ya Wahadhiri kulingana na bajeti ya fedha kwa mwezi na mwaka husika.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved