Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 9 | Sitting 7 | Works, Transport and Communication | Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi | 99 | 2022-11-08 |
Name
Mussa Ramadhani Sima
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Singida Mjini
Primary Question
MHE. MUSSA R. SIMA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaanza kujenga Kiwanja cha Ndege Singida Mjini?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mussa Ramadhani Sima, Mbunge wa Singida Mjini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Kiwanja cha Ndege cha Singida kilifanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ufadhili wa Benki ya Dunia mwaka 2017 kupitia mradi wa Transport Sector Support Project (TSSP) kwa ajili ya upanuzi na ukarabati wa Kiwanja hiki cha Ndege.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea kutafuta fedha kutoka vyanzo vya Ndani na Washirika wa Maendeleo ili kuanza ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Singida.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved