Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 9 | Sitting 8 | Foreign Affairs and International Cooperation | Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki | 112 | 2022-11-09 |
Name
Felista Deogratius Njau
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. FELISTA D. NJAU aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaajiri Maafisa Habari katika Balozi zetu ili kuutangaza nchi na vivutio mbalimbali?
Name
Amber. Mbarouk Nassor Mbarouk
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nominated
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Felista Deogratius Njau, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kulijulisha Bunge lako Tukufu kuwa Maofisa wanaopelekwa Ubalozini, moja ya majukumu yao ya msingi ni kutekeleza Sera ya Mambo ya Nje ambayo imeweka msisitizo katika kutekeleza Diplomasia ya Uchumi. Miongoni mwa majukumu ya kila Ofisa na kila Ubalozi ni pamoja na kutangaza vivutio vya utalii wetu, kubidhaisha Kiswahili, kuvutia wawekezaji na kutafuta fursa za masoko kwa bidhaa zetu. Aidha, Wizara ina utaratibu wa kuwajengea Watumishi uwezo kupitia mafunzo ili waweze kufanya kazi zaidi ya moja ikiwemo kuwa na uwezo wa kutoa habari muhimu kwa wadau.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved