Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 9 | Sitting 8 | Works, Transport and Communication | Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi | 118 | 2022-11-09 |
Name
Salim Alaudin Hasham
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ulanga
Primary Question
MHE. ALAUDIN H. SALIM aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itafungua barabara ya kimkakati inayotoka Mahenge mpaka Liwale kupitia Malinyi, Mlimba, Njombe na Songea?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI (MHE. ENG. GODFREY K. MSONGWE) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Alaudin Hasham Salim, Mbunge wa Ulanga, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Barabara inayotoka Mahenge kwenda Liwale ni Mahenge - Mwaya – Ilonga – Liwale ambapo sehemu ya Mahenge hadi Ilonga imefunguliwa na inapitika majira yote ya mwaka. Hata hivyo, kutoka Ilonga kwenda Liwale hakuna barabara kwa Mwalimu Nyerere na itahitaji kufanyiwa upembuzi yakinifu wa awali kuona iwapo inakidhi vigezo vya mazingira kabla ya kufunguliwa.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved