Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 9 | Sitting 8 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 121 | 2022-11-09 |
Name
Oran Manase Njeza
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbeya Vijijini
Primary Question
MHE. ORAN M. NJEZA aliuliza: -
Je ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Ndaki ya Sayansi ya Afya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Mamlaka ya Mji wa Mbalizi?
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, napenda kujibu swali na Mheshimiwa Oran Manase Njeza, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimeanza hatua za awali kwa kuwasilisha kwa Msajili wa Hazina maombi ya kupewa ardhi yenye ukubwa wa hekari 2000 kwenye eneo lililokuwa shamba la Tanganyika Packers kwa ajili ya ujenzi. Kwa sasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinaendelea kufuatilia maombi haya kwa Msajili wa Hazina.
Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa Ndaki ya Sayansi ya Afya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam - Mbalizi utaanza mara moja pale upatikanaji wa ardhi utakapokamilika.
Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved