Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 9 | Sitting 8 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 122 | 2022-11-09 |
Name
Hussein Nassor Amar
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nyang'hwale
Primary Question
MHE. HUSSEIN N. AMAR aliuliza: -
Je, kuna mpango gani wa kujenga Chuo cha VETA Nyangh’wale?
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, naomba sasa kujibu swali la Mheshimiwa Hussein Nassor Amar, Mbunge wa Jimbo la Nyangh’wale, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inayo azma ya kujenga Chuo cha Ufundi Stadi katika kila Mkoa na Wilaya nchini. Katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali imetenga kiasi cha Shilingi bilioni 100 kwa ajili ya kujenga Vyuo vya VETA katika Wilaya 63 ambazo hazina vyuo hivyo. Kiasi hiki kitatumika pia katika ujenzi wa Chuo cha VETA katika Mkoa wa Songwe.
Mheshimiwa Naibu Spika, Nyangh’wale ni miongoni mwa Wilaya 63 ambazo zipo kwenye mpango wa kujengewa Vyuo vya Ufundi Stadi kwa mwaka huu wa fedha.
Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved