Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 7 | Sitting 8 | Defence and National Service | Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga taifa | 70 | 2022-04-19 |
Name
Daimu Iddi Mpakate
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduru Kusini
Primary Question
MHE. DAIMU I. MPAKATE aliuliza: -
Je, Serikali haioni haja ya kurejesha Kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Tunduru ili kuimarisha ulinzi?
Name
Dr. Stergomena Lawrence Tax
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Nominated
Answer
WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA alijibu: -
Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Daimu Iddi Mpakate, Mbunge wa Tunduru Kusini, kama iufatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wa kuimarisha ulinzi katika mipaka ikiwa ni pamoja na mpaka wa Kambi ya Wananchi wa Jeshi la Tanzania Tunduru na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ipo katika mchakato wa kurejesha Kambi ya Jeshi la Wananchi Wilayani Tunduru. Tayari Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imekwishaomba fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kambi hiyo toka Wizara ya Fedha na Mipango.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved