Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 7 | Sitting 7 | Community Development, Gender and Children | Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum | 59 | 2022-04-14 |
Name
Husna Juma Sekiboko
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ZAINAB A. KATIMBA K.n.y. MHE. HUSNA J. SEKIBOKO aliuliza: -
Je, kuna athari gani za kijamii kwa watumishi wenza kuishi mbali na watoto wao?
Name
Mwanaidi Ali Khamis
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Husna Juma Sekiboko, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, familia ni taasisi muhimu sana katika kuleta ustawi kwa jamii na Taifa kwa ujumla. Ni kweli kuwa yapo madhara ya kijamii kwa watumishi wenza kuishi mbali na watoto wao madhara hayo ni kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kuongezeka kwa vitendo vya ukatili kwa watoto majumbani; kukosa malezi chanya inayopelekea watoto kuathirika kisaikolojia; watoto kutokupata lishe bora inayopelekea udumavu na mmomonyoko wa maadili na kuvunjika kwa ndoa kunakosababisha watoto wa mtaani. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved