Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 10 | Sitting 1 | Youth, Disabled, Labor and Employment | Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu | 1 | 2023-01-31 |
Name
Dr. Thea Medard Ntara
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. THEA M. NTARA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itatangaza kima cha chini cha mishahara kwa Wafanyakazi wa Serikali na mashirika binafsi?
Name
Paschal Katambi Patrobas
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Shinyanga Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCAL P. KATAMBI) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Thea Medard Ntara, Mbunge wa Viti Maalum kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, ninapenda kulijulisha Bunge lako tukufu kuwa kima cha chini cha mshahara kwa sekta ya umma kilitangazwa tarehe 13/5/2022 na utekelezaji wake ulianza tarehe 1 Julai, 2022. Kwa upande wa sekta binafsi kima cha chini cha mshahara kilitangazwa tarehe 25/11/2022 kwenye Gazeti la Serikali Na. 687 baada ya Bodi ya Kima cha Chini cha Mishahara kukamilisha utafiti na kutoa mapendekezo ya viwango kwa Sekta Binafsi ambayo yaliridhiwa na Baraza la Ushauri kuhusu Kazi, Uchumi na Jamii (LESCO). Utekelezaji wake unaanza rasmi Tarehe 1 Julai, 2023.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved