Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 10 | Sitting 1 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Waziri wa Mifugo na Uvuvi | 7 | 2023-01-31 |
Name
Bupe Nelson Mwakang'ata
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. BUPE N. MWAKANG’ATA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itajenga josho katika Kata ya Miula Wilayani Nkasi?
Name
Abdallah Hamis Ulega
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkuranga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI aljibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Bupe Nelson Mwakang’ata, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/2022, Wizara ilipeleka kiasi cha shilingi milioni 108 kwa ajili ya ujenzi wa majosho sita katika Hamashauri ya Nkasi katika Vijiji vya Kipande, Katani, Chala, Mikukwe, Chalatila na Sintali. Majosho hayo yapo katika hatua mbalimbali za ujenzi.
Mheshimiwa Spika, Wizara inaendelea kuwasiliana na Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi ili kukamilisha ujenzi wa majosho hayo na kutoa fursa kwa Serikali kutenga fedha zaidi kwa ajili ya ujenzi wa majosho mengine Nkasi Kusini ikiwemo Kata ya Miula. Aidha, Serikali inaendelea kuhamasisha wafugaji kuchangia ujenzi wa miundombinu ya mifugo ikiwemo majosho katika maeneo yao. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved