Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 10 | Sitting 1 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 19 | 2023-01-31 |
Name
Hawa Mchafu Chakoma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HAWA M. CHAKOMA aliuliza: -
Je, ni wanafunzi wangapi waliokuwa wajawazito na wangapi wamerejeshwa shuleni baada ya agizo la Mheshimiwa Rais?
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -
Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Hawa Mchafu Chakoma Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2021/2022 wanafunzi wa shule za msingi waliopata ujauzito ni 1,554 na sekondari ni 7,457.
Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwezi Januari, 2023 wanafunzi waliorejea shuleni baada ya kukatiza masomo kwa sababu ya ujauzito na kuendelea na masomo ya elimu ya sekondari ni 1,692. Aidha, kwa upande wa shule za msingi Serikali inaendelea kukusanya taarifa za wanafunzi waliorejea shuleni baada ya kukatiza masomo kwa sababu ya ujauzito. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved