Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 10 | Sitting 2 | Energy and Minerals | Wizara ya Nishat | 29 | 2023-02-01 |
Name
Hawa Subira Mwaifunga
Sex
Male
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HAWA S. MWAIFUNGA aliuliza: -
Je, ni nini mkakati wa Serikali kuondoa kero ya ukatikaji wa umeme nchini hasa katika maeneo ya biashara kama Kariakoo?
Name
Stephen Lujwahuka Byabato
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bukoba Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Hawa Subira Mwaifunga, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuondoa tatizo la ukatikaji umeme Nchini, Serikali imebuni na imeanza utekelezaji wa Mradi kabambe wa Gridi Imara unaolenga kuboresha upatikanaji wa umeme nchini kwa kufanya uboreshaji mkubwa kwenye miundombinu ya kusafirisha na kusambaza umeme. Katika mradi huo, pamoja na kazi nyingine, jumla ya kilomita zipatazo 3,930 za njia za kusafirisha umeme zitajengwa, jumla ya vituo vikubwa vya kupoza umeme 62 vitajengwa na kilomita zipatazo 2,572 za njia za usambazaji umeme zitajengwa. Katika kutekeleza mradi huu, Serikali imetenga jumla ya shilingi bilioni 500 kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kutatua changamoto ya upungufu wa umeme nchini, Serikali inaendelea na jitihada za kuongeza uzalishaji umeme kupitia vyanzo mbalimbali kama vile gesi, maji, umeme jua na upepo. Miradi hiyo iko kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji. Inatarajiwa kuwa, utekelezaji wa miradi hiyo utakapokamilika, utaondoa kabisa kero ya ukatikaji wa umeme nchini. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved