Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 10 | Sitting 4 | Youth, Disabled, Labor and Employment | Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu | 49 | 2023-02-03 |
Name
Fakharia Shomar Khamis
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kutoa elimu kwa vijana walio mashuleni juu ya kujikinga na dawa za kulevya?
Name
Paschal Katambi Patrobas
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Shinyanga Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCAL P. KATAMBI) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Fakharia Shomar Khamis, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeandaa na kuzindua Mwongozo wa Utoaji Elimu Kuhusu Dawa za Kulevya nchini ambao ulizinduliwa tarehe 2 Julai, 2022 na Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwenye kilele cha siku ya Taifa ya Kupinga Dawa za Kulevya, Jijini Dar es Salaam. Mwongozo huo tayari umeanza kutumika kuelimishia walimu wa shule za msingi na sekondari pamoja na asasi za kiraia zinazojihusisha na utoaji wa elimu kwa makundi mbalimbali ya jamii wakiwemo vijana waliopo mashuleni, juu ya tatizo la dawa za kulevya nchini.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved