Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 10 | Sitting 5 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 81 | 2023-02-06 |
Name
Bahati Keneth Ndingo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Mbarali
Primary Question
MHE. BAHATI K. NDINGO aliuliza: -
Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwajengea uwezo Wahitimu wa Vyuo nchini ili waweze kushindana katika soko la ajira?
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Bahati Keneth Ndingo, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi ujulikanao kama, Higher Education for Economic Transformation (HEET), inaendelea na maandalizi ya uboreshaji wa mitaala iliyopo na uandaaji wa mitaala mipya zaidi ya 290 katika programu za kipaumbele cha Taifa ili kuwajengea uwezo wahitimu kuhimili ushidani wa soko la ajira ndani na nje ya nchi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hatua inayoendelea ni ukusanyaji wa maoni (tracer study and needs assessment) kutoka kwa wadau mbalimbali wa elimu ili kubaini mahitaji halisi. Mitaala hiyo iliyoboreshwa inatarajiwa kuanza kutumika katika mwaka wa masomo 2023/2024, nakushukuru.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved