Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 10 | Sitting 5 | Community Development, Gender and Children | Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum | 85 | 2023-02-06 |
Name
Esther Nicholus Matiko
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTHER N. MATIKO aliuliza: -
Je, ni kwa nini Serikali isianzishe madawati ya kijinsia katika ngazi za Kata na Vijiji kutokana na ongezeko la vitendo vya ukatili?
Name
Mwanaidi Ali Khamis
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamaii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Esther Nicholus Matiko Mbunge wa viti maalumu kama ifuatvyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua umuhimu wa kudhibiti vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii ambapo imeratibu uanzishwaji wa madawati 420 ya Jinsia katika vituo vya Jeshi la Polisi, na 153 vya Jeshi la Magereza. Aidha, madawati ya ulinzi wa watoto yameanzishwa katika shule za msingi na sekondari. Vile vile, madawati ya jinsia yanaanzishwa kwenye vyuo vyote nchini pamoja na maeneo ya umma kama kwenye masoko. Kwa upande mwingine, kKamati za Ulinzi wa Wanawake na Watoto zimeanzishwa katika ngazi ya mtaa/vijiji hadi Taifa kwa asilimia 88. Madawati haya yanachangia kwa kiasi kikubwa katika kushughulikia masuala ya ukatili wa kijinsia katika jamii. Ahsante
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved